Pages

Sunday, 12 November 2017

JINA LA MUNGU WA ISRAELI (YHWH)


Yahweh Mungu katika Kiyahudi, Mungu kama alivyoelewa katika majadiliano ya kiiolojia ya Kiyahudi. Bwana, mungu wa kitaifa wa falme za kale za Israeli na Yuda. Tetragrammaton, herufi nne za Kiebrania YHWH kama jina la Mungu, na matamshi mbalimbali waliyopewa.

Wayahudi wanasema kwamba YHWH, mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo na mungu wa kitaifa wa Waisraeli, aliwaokoa Waisraeli kutoka utumwa Misri, na akawapa Sheria ya Musa kwenye Mlima wa Sinai wa Biblia kama ilivyoelezwa katika Torati. ... Katika jadi za Kiyahudi jina jingine la Mungu ni Elohim.

Bwana, mungu wa Waisraeli, ambaye jina lake limefunuliwa kwa Musa kama maandishi nne ya Kiebrania (YHWH) aitwaye tetragrammatoni. Baada ya Uhamisho wa Babiloni (bne karne ya 6), na hasa kutoka karne ya 3 bce juu, Wayahudi waliacha kutumia jina Yahweh kwa sababu mbili.
Kama Wayahudi walipokuwa wanadamu badala ya dini ya ndani tu, jina la kawaida zaidi Elohim, linamaanisha "Mungu," lilikuwa limefanyika badala ya Bwana kuonyesha uhuru wa ulimwengu wote wa Mungu wa Israeli juu ya wengine wote. Wakati huo huo, jina la Mungu lilizidi kuonekana kuwa takatifu sana kutamka; kwa hiyo ilikuwa kubadilishwa kwa sauti katika ibada ya sinagogi na neno la Kiebrania Adonai ("Bwana wangu"), ambalo lilitafsiriwa kama Kyrios ("Bwana") katika Septuagint, tafsiri ya Kiyunani ya Maandiko ya Kiebrania.
Masoretes, ambao kutoka karne ya 6 hadi karne ya 10 walifanya kazi ya kuzaliana maandishi ya awali ya Biblia ya Kiebrania, badala ya matoleo ya jina la YHWH na ishara ya vidole vya maneno ya Kiebrania Adonai au Elohim. Wataalam wa Kikristo wanaozungumza Kilatini walibadilishana Y (ambayo haipo katika Kilatini) na mimi au J (mwisho wa ambayo iko katika Kilatini kama aina ya I). Kwa hiyo, tetragrammatoni ikawa jina la Kilatini jina la Yehova (JeHoWaH). Kama matumizi ya jina yalienea katika Ulaya yote ya kale, barua ya awali ya J ilikatamka kulingana na lugha ya lugha ya kawaida badala ya Kilatini.

Ingawa wasomi wa Kikristo baada ya kipindi cha Renaissance na Kipinduzi walitumia neno Yehova kwa YHWH, karne ya 19 na 20 karne ya wasomi wa Biblia tena walianza kutumia fomu Yahweh. Waandishi wa Kikristo wa awali, kama vile Mtakatifu Clement wa Alexandria katika karne ya 2, walitumia fomu kama Yahweh, na matamshigrammaton hii hayakuwahi kupotea. Matoleo mengi ya Kiyunani pia yalionyesha kuwa YHWH inapaswa kutamkwa Yah Maana ya jina la kibinafsi la Mungu wa Israeli limefasiriwa kwa njia mbalimbali. Wataalamu wengi wanaamini kwamba maana sahihi zaidi inaweza kuwa "Yeye huleta ndani ya uwepo wowote uliopo" (Yahweh-Asher-Yahweh).


Jina la kibinadamu la Mungu labda likajulikana muda mrefu kabla ya wakati wa Musa. Jina la mama ya Musa lilikuwa Jokebed (Yokheved), neno linalojulikana kwa Yahweh. Kwa hiyo, kabila la Lawi, ambalo Musa alikuwa mali yake, labda alijua jina Yahweh, ambalo hapo awali lilikuwa (kwa njia yake fupi Yo, Yah, au Yahu) kuomba kidini kwa maana isiyo sahihi iliyotokana na utukufu wa ajabu na wa ajabu wa udhihirisho wa takatifu


Wayahudi wanaamini kuwa kuna Mungu mmoja ambaye sio tu aliyeumba ulimwengu, lakini ambaye kila Myahudi anaweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi na binafsi. Wanaamini kwamba Mungu anaendelea kufanya kazi duniani, akiathiri kila kitu ambacho watu hufanya. Uhusiano wa Kiyahudi na Mungu ni uhusiano wa agano
JINA KAMILI LA MUNGU NI NIKO  AMBAYE NIKO KAMA ALIVYO JIFUNUA KWA MUSA  ZAIDI YA YOTE YESU ALISEMA KUA YEYE NI MUNGU WA IBRAHIMU ISAKA NA YAKOBO MUNGU WA WALIO HAI.
BARIKIWA PASIPO MWISHO MILELE NA MILELE AMINA.     

ISAYA 1

Isaya 1

1  Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi, aliyoyaona katika habari za Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia na Yothamu na Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.
2  Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana Bwana amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi.
3  Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.
4  Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha Bwana, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.
5  Mbona mnataka kupigwa hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.
6  Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwa-zongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.
7  Nchi yenu ni ukiwa; miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu, wageni wameila mbele ya macho yenu; nayo ni ukiwa, kana kwamba imeangamizwa na wageni.
8  Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama kipenu katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa.
9  Kama Bwana wa majeshi asingalituachia mabaki machache sana, tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana na Gomora.
10  Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.
11  Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume.
12  Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu?
13  Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
14  Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua.
15  Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
16  Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
17  jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
18  Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
19  Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
20  bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
21  Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki; haki ilikaa ndani yake, bali sasa wauaji!
22  Fedha yako imekuwa takataka, divai yako imechanganywa na maji.
23  Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wevi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawawasilii.
24  Kwa hiyo, asema Bwana, Bwana wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitatwaa kisasi kwa adui zangu;
25  nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote;
26  nami nitarejeza upya waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu.
27  Sayuni itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki.
28  Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa.
29  Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
30  Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji.
31  Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima.

KRISTO YESU HUSAMEHE


Ni dhahiri kuwa tunatenda dhambi kiasi ambacho tunaona atuwezi samehewa kabisa kutokana na maovu yetu, ni hakika wanadamu tu wadhambi na hakika yake twatenda dhambi kila iitwapo leo
dhambi ni kutenda kinyume na mapenzi ya MUNGU kutenda neno lolote lisilo haki na kudhamiria kulitenda lisilo haki
Dhambi hututenga wanaadamu na MUNGU
                                     
kwa sasa dhambi zimeshamiri kiasi kwamba dhambi nyingine huonekana za kawaida  lakini daima dhambi ni dhambi na MUNGU uhukumu kwa haki
kuwazia dhambi ni dhambi kudhamiria kutenda dhambi ni dhambi maana imeandikwa

 Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."

hakuna aliye mkamilifu hata kwetu sisi wanadamu ivyo nivema kujijengea utamaduni wa kutubu.
 dhambi ni dhambi umekosa katika moja wakosa juu ya yote


HUSAMEHE YOTE

imeandikwa ISAYA 1: 4  4  Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha Bwana, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.
  
hivyo ni vema kutubu  nae bwana wa majeshi husamehe  maana imeandikwa
ISAYA  1:18   Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
MUNGU WA IBRAHIMU ISAKA NA YAKOBO  NI WINGI WA REHEMA, HURUMA NA MSAMAHA  UPENDO NA UPOLE  WA HAKI NA WAKWELI
MUNGU ahangalii wingi wa dhambi au dhambi gani ulitenda uangalia unyenyekevu wa moyo na ukubali wa mtu kutubu

UTUBUPO AMINI UMESAMEHEWA .            
                                                                           Mariamu alikuwa ameonwa kama mwenye dhambi mkuu, lakini Kristo alijua mazingira ambayo yalitengeneza maisha yake. Angeweza kuzima kila cheche ya matumaini moyoni mwake, lakini hakufanya hivyo. Ni yeye aliyemwinua kutoka katika kukata tamaa na uharibifu. Mara saba alikuwa amemsikia Yesu akikemea mapepo ambayo yalitawala moyo na akili yake. Alikuwa amesikia vilio vya nguvu kwa Baba kwa niaba yake. Mariamu alijua jinsi dhambi ilivyokuwa chukizo kwa utakatifu wake ambao haukuyumba na kwa nguvu zake alikuwa ameshinda. Wakati suala lake lilipoonekana kutokuwa na tumaini kwa watu, Kristo alimwona Mariamu akiwa na uwezo kwa ajili ya kutenda mema. Aliona mienendo iliyo bora ya tabia yake. Mpango wa wokovu umewekeza kwa binadamu uwezekano mkubwa sana na uwezekano huu ulikuwa uonekane kwa Mariamu. Kupitia kwa neema yake, akawa mshirika wa tabia ya Mungu. Yeye aliyekuwa ameanguka na ambaye akili yake iliwahi kuwa makazi ya mapepo, aliletwa karibu sana na Mwokozi katika ushirika na huduma. Alikuwa ni Mariamu huyu ambaye aliketi na kujifunza kwake. Ni Mariamu huyu ambaye alimimina mafuta ya thamani kichwani pa Yesu na kuosha miguu yake kwa machozi yake. Mariamu alisimama kando ya msalaba na kumfuata hadi kaburini. Mariamu alikuwa wa kwanza baada ya ufufuo. Ni Mariamu ambaye alianza kumtangaza Mwokozi aliyefufuka.

Yesu anajua mazingira ya kila nafsi. Unaweza kusema, mimi ni mwovu, mwovu sana. Unaweza ukawa uko hivyo; lakini kadiri ulivyo mbaya, ndivyo unavyomhitaji Yesu zaidi. Kamwe hamkatai mtu yeyote anayelia, anayetubu. Hamwambii yeyote yale yote anayoweza kuyafunua, bali anasihi kila nafsi yenye hofu kuwa jasiri. Atawasamehe bure wote wanaomjia yeye kwa ajili ya msamaha na urejeshwaji…. Leo anasimama kwenye madhabahu ya uvumba, akimwasilishia Mungu maombi ya wale wanaotamani msaada wake.

Yesu huinua roho zao wanaomgeukia kama kimbilio, juu ya wanaoshitaki na ugomvi wa ndimi za watu. Hakuna mtu au malaika waovu wanaoweza kushitaki roho hizi. Kristo huwaunganisha na tabia yake mwenyewe ya kimbingu. Huwa wanasimama kando ya Mbeba dhambi mkuu, katika nuru inayotoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu.

ZAIDI YA YOTE USITENDE TENA DHAMBI WALA KUURUDIA UOVU WAKO WA ZAMANI IMARIKA NA YEYE ALIYE MWEZA WA YOTE NA AKUSAIDIE

HERI NA UMEBARIKIWA WEWE  UMTAFUTAE SANA MUNGU 

Saturday, 8 April 2017

WIMBO WA MUSA NA MWANAKONDOO



                           
*WIMBO WA MUSA NA MWANAKONDOO*



*_Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. Kutoka 15:2._*


⚜Kutoka kwenye hatari kubwa, usiku mmoja ulileta ukombozi mkamilifu. Kundi kubwa, lililohitaji msaada – wanaume watumwa ambao hawakuzoea vita, wanawake, watoto na ng’ombe, bahari ikiwa mbele zao na majeshi yenye nguvu ya Misri yakiendelea kuwakaribia kutokea nyuma – umati huu ulishuhudia njia yao ikifunguka kwenye maji na adui zao wakishindwa katika hatua waliyotarajia kushinda. Ni Yehova pekee aliyewaletea ukombozi na mioyo yao iligeuziwa kwake ikiwa na shukrani na imani. Msisimko wao uliwafikishia kwenye nyimbo za sifa.

⚜Roho wa Mungu alikaa juu ya Musa naye akaongoza watu katika wimbo mkuu wa ushindi wa shukrani, moja kati zile za awali na za utukufu mkubwa zaidi zinazofahamika kwa watu…

⚜Wimbo sio wa Wayahudi peke yao. Unaelekeza mbele kwenye maangamivu ya maadui wote wa haki na ushindi wa mwisho wa Israeli ya Mungu. Nabii wa Patmo aliona umati wa watu waliovaa mavazi meupe “wenye kushinda,” nao “walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo” (Ufunuo 15:2,3)…

⚜Katika kuziweka huru roho zetu kutoka kwenye utumwa wa dhambi, Mungu ametupatia ukombozi ulio mkuu kuliko ule wa Waebrania kwenye Bahari nyekundu. Kama jeshi la Waebrania, inatupasa tumsifu Bwana kwa moyo na nafsi na sauti kwa sababu ya “maajabu yake kwa wanadamu.” Wale wanaodumu kwenye rehema kuu za Mungu na huku wakifikiria juu ya karama zake ndogo, watafunga mkanda wa furaha na kutunga wimbo mioyoni mwao kwa ajili ya Bwana. Baraka za kila siku tunazopokea kutoka mkononi mwa Mungu na zaidi ya yote kifo cha Yesu kwa ajili ya kuleta furaha na mbingu karibu nasi, yapasa liwe neno kuu kwa ajili ya shukrani isiyokoma…

⚜Wakazi wote wa mbinguni wanaungana katika kumsifu Mungu. Hebu tujifunze wimbo wa malaika sasa, ili tupate kuuimba tutakapojiunga na safu yao inayong’aa.

Kwa Walio Uhamishoni

Tarehe 2/4/2017

*Kwa Walio Uhamishoni*



▶Iwapo ungepewa kipande cha karatasi kinachoanza kwa neno, “Mheshimiwa,” ungetambua kwamba unasoma barua. Na ungedhani kuwa barua ile ilitoka kwa mtu fulani ambaye huenda hukuwa karibu naye.

▶Kama zilivyo barua za kisasa kwamba zina kanuni ya kuanza, ndivyo zilivyokuwa barua zile za kale. Kwanza Petro anaanza kama vile ambavyo mtu ye yote wa kale angelianza. Inamtambulisha mwandishi na wale ambao ilitumwa kwao.

▶Soma 1 Petro 1:1. Tunaweza kujifunza kitu gani kutoka katika aya hii moja ambacho kitatusaidia kupata sehemu ndogo ya muktadha?



▶Petro anajitambulisha kwa uwazi. Jina lake ndilo neno la kwanza katika barua hii. Hata hivyo, mara moja anajitambulisha kama “mtume wa Yesu Kristo.” Kwa hiyo, kama vile Paulo alivyofanya mara kwa mara (Wagalatia 1:1, Warumi 1:1, Waefeso 1:1), Petro mara moja anathibitisha “sifa” zake, akisisitiza mwito wake mtakatifu. Alikuwa ni “mtume,” yaani “mtu aliyetumwa,” na aliyemtuma ni Bwana Yesu Kristo.

▶Petro anatambulisha eneo ambalo barua yake ilielekezwa: Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia. Haya yote ni maeneo ndani ya Asia Ndogo, karibu sawa na eneo la Uturuki ya leo mashariki ya mlango wa bahari wa Bosporus.

▶Zipo hoja kuhusu iwapo Petro alikuwa akiandika zaidi kwa waumini wa Kiyahudi au kwa waumini wa-Mataifa. Maneno anayotumia Petro katika 1 Petro 1:1 “Utawanyiko/wageni,” ni maneno ambayo kwa asili yanawahusu Wayahudi waliokuwa wakiishi nje ya Nchi Takatifu katika karne ya kwanza. Maneno kuteuliwa(BHN) na kutakaswa katika 1 Petro 1:2 yanafaa kwa wote Wayahudi na Mataifa. Kuwaeleza wale ambao wako nje ya jumuia kuwa ni “Mataifa” (1 Petro 2:12; 4:3) pia husisitiza tabia ya Kiyahudi ya wale ambao Petro anawaandikia.

▶Wafasiri wengine wanatoa hoja, kwa kujibu, kwamba kile Petro anachokisema katika 1 Petro 1:18;4:3 kingekuwa sahihi zaidi kusemwa kuhusu waongofu wa Mataifa wanaoingia katika Ukristo kuliko kwa wale wa Kiyahudi. Hata hivyo, je Petro angeweza kweli kuwaandikia Wayahudi kuhusu “mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;”? Au je angeweza kusema kwa wasomaji Wayahudi, “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali” (1 Petro 4:3)?

▶Hata hivyo, kilicho cha maana sana kwetu si nani aliandikiwa, bali, kile ambacho ujumbe unasema.
🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚

SHERIA YA MUNGU ISIYOBADILIKA




                                                         KIOO CHA AJABU.
                                     (SHERIA YA MUNGU ISIYOBADILIKA)

FUNGU KUU: “Sheria ya BWANA ni kamilifu, huiburudisha nafsi, Ushuhuda wa BWANA ni amini, humtia mjinga hekima”. Zab 19:7
Ni jambo la pekee na lenye faida kubwa kuwa,mtu aishikaye sheria ya Mungu anakuwa ni mwenye amani, furaha na mwenye uhakika wa kuuingia mji mtakatifu – Mbinguni.

‘Twaweza kujiuliza nini maana ya sheria………….?’

Sheria ni utaratibu, agizo au mwongozo wenye mamlaka uliotolewa na mwenye mamlaka kwa ajili ya kutoa maelezo sahihi kwa jamii katika kuelekeza, kusimamia, kukosoa na kuadibisha.
Sheria ya Mungu inafananishwa na kioo kwa maana hii kuwa,ina uwezo wa kuonyesha bayana / kwa usahihi uovu au makosa ya mwanadamu. Kwa sababu sheria yake ni kamilifu, inaonesha kwa usahihi usiokuwa na shaka yoyote kuwa dhambi ni hii na utakatifu ni huu. Yakobo 1:23, Warumi 2:13

Ila sheria yenyewe haina uwezo wa kuondoa dhambi/makosa – kama kioo kilivyo.
Maneno haya: sheria, Amri na torati katika maandiko matakatifu (Biblia) wakati mwingine hutumika katika ulinganifu au kwa maana sawasawa.
 Mfano. Soma aya hizi; Zab. 19:7, 1Yoh 5:3, Rum 7:7, Zab1:2, Yoh 14:15.

KAZI ZA SHERIA
Ndugu zangu wapendwa ninapenda tufahamu kuwa sheria ya Mungu ina kazi hizi zifuatazo (japo waweza kufahamu ngingi zaidi);
1.  Kuifanya dhambi ionekane/kuitambulisha dhambi. Rum 7:7-13
2.  Kutuongoza kwa Kristo (Sheria ni kiongozi) Gal. 3:24

SHERIA NA NEEMA
Ni kweli kuwa tunaokolewa kwa neema, ambayo hutuongoza kuikataa dhambi. Na hatuwezi kuitambua dhambi pasipokuwa na sheria.Naam, sheria huionesha/funua  dhambi  na Neema ya Kristo huiondoa. Tito 2:11-12.
MAKUNDI YA SHERIA
Katika Biblia, sheria yaweza kufundishwa katika namna nyingi au makundi tofautitofauti.
Hebu tuyatazame makundi makuu haya mawili.
(1). Sheria zilizoandikwa na Mungu, muumba wa mbingu na nchi.
(sheria/amri 10 za Mungu)
(2). Sheria zilizoandikwa na Musa, Nabii wa Mungu
(sheria za maagizo).

SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO. JIHADHARI NA ONYEKA!

*SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO.       JIHADHARI NA ONYEKA!.*


*JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*

 *1.Usichelewe kwenda HAJA.*    Kutunza mkojo kweye kibofu chako  kwa muda mrefu ni wazo baya.                      Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu.                     Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu  huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha  maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
 *2. Kula Chumvi kupita kiasi.* Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.
 *3. Kula nyama kupita kiasi.*
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia-  sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi  inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4. *Unywaji mwingi wa "Caffeins".*
 Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k.                              Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango  cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
*5. Kutokunywa maji.*
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri.                           Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha  kutosha kutoa kwa njia ya figo.                        *** Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
     Kuna njia rahisi ya kuangalia kama  unakunywa maji ya kutosha:                         Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
*6. Kuchelewa matibabu.*
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara.                            Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe... Shirikisha wengine, kama unajali.               ----------------
*Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:*
D- baridi*
 Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
 Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
 MWISHO... Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
*Inaweza kumsaidia mtu!*


Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.

*Maonyo muhimu ya Afya*
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio  la kushoto.
 2. Usinywe  dawa zako kwa maji baridi....
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
 6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
 7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
 Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako....!!.