(SHERIA YA MUNGU ISIYOBADILIKA)
FUNGU KUU: “Sheria ya BWANA ni kamilifu, huiburudisha nafsi, Ushuhuda wa BWANA ni amini, humtia mjinga hekima”. Zab 19:7
Ni jambo la pekee na lenye faida kubwa kuwa,mtu aishikaye sheria ya Mungu anakuwa ni mwenye amani, furaha na mwenye uhakika wa kuuingia mji mtakatifu – Mbinguni.
‘Twaweza kujiuliza nini maana ya sheria………….?’
Sheria ni utaratibu, agizo au mwongozo wenye mamlaka uliotolewa na mwenye mamlaka kwa ajili ya kutoa maelezo sahihi kwa jamii katika kuelekeza, kusimamia, kukosoa na kuadibisha.
Sheria ya Mungu inafananishwa na kioo kwa maana hii kuwa,ina uwezo wa kuonyesha bayana / kwa usahihi uovu au makosa ya mwanadamu. Kwa sababu sheria yake ni kamilifu, inaonesha kwa usahihi usiokuwa na shaka yoyote kuwa dhambi ni hii na utakatifu ni huu. Yakobo 1:23, Warumi 2:13
Ila sheria yenyewe haina uwezo wa kuondoa dhambi/makosa – kama kioo kilivyo.
Maneno haya: sheria, Amri na torati katika maandiko matakatifu (Biblia) wakati mwingine hutumika katika ulinganifu au kwa maana sawasawa.
Mfano. Soma aya hizi; Zab. 19:7, 1Yoh 5:3, Rum 7:7, Zab1:2, Yoh 14:15.
KAZI ZA SHERIA
Ndugu zangu wapendwa ninapenda tufahamu kuwa sheria ya Mungu ina kazi hizi zifuatazo (japo waweza kufahamu ngingi zaidi);
1. Kuifanya dhambi ionekane/kuitambulisha dhambi. Rum 7:7-13
2. Kutuongoza kwa Kristo (Sheria ni kiongozi) Gal. 3:24
SHERIA NA NEEMA
Ni kweli kuwa tunaokolewa kwa neema, ambayo hutuongoza kuikataa dhambi. Na hatuwezi kuitambua dhambi pasipokuwa na sheria.Naam, sheria huionesha/funua dhambi na Neema ya Kristo huiondoa. Tito 2:11-12.
MAKUNDI YA SHERIA
Katika Biblia, sheria yaweza kufundishwa katika namna nyingi au makundi tofautitofauti.
Hebu tuyatazame makundi makuu haya mawili.
(1). Sheria zilizoandikwa na Mungu, muumba wa mbingu na nchi.
(sheria/amri 10 za Mungu)
(2). Sheria zilizoandikwa na Musa, Nabii wa Mungu
(sheria za maagizo).
No comments:
Post a Comment