
dhambi ni kutenda kinyume na mapenzi ya MUNGU kutenda neno lolote lisilo haki na kudhamiria kulitenda lisilo haki
Dhambi hututenga wanaadamu na MUNGU

kwa sasa dhambi zimeshamiri kiasi kwamba dhambi nyingine huonekana za kawaida lakini daima dhambi ni dhambi na MUNGU uhukumu kwa haki
kuwazia dhambi ni dhambi kudhamiria kutenda dhambi ni dhambi maana imeandikwa
Mathayo 5:27 -28 "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini moyoni mwake."
hakuna aliye mkamilifu hata kwetu sisi wanadamu ivyo nivema kujijengea utamaduni wa kutubu.
dhambi ni dhambi umekosa katika moja wakosa juu ya yote
HUSAMEHE YOTE

hivyo ni vema kutubu nae bwana wa majeshi husamehe maana imeandikwa
ISAYA 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
MUNGU WA IBRAHIMU ISAKA NA YAKOBO NI WINGI WA REHEMA, HURUMA NA MSAMAHA UPENDO NA UPOLE WA HAKI NA WAKWELI
MUNGU ahangalii wingi wa dhambi au dhambi gani ulitenda uangalia unyenyekevu wa moyo na ukubali wa mtu kutubu
UTUBUPO AMINI UMESAMEHEWA .

Yesu anajua mazingira ya kila nafsi. Unaweza kusema, mimi ni mwovu, mwovu sana. Unaweza ukawa uko hivyo; lakini kadiri ulivyo mbaya, ndivyo unavyomhitaji Yesu zaidi. Kamwe hamkatai mtu yeyote anayelia, anayetubu. Hamwambii yeyote yale yote anayoweza kuyafunua, bali anasihi kila nafsi yenye hofu kuwa jasiri. Atawasamehe bure wote wanaomjia yeye kwa ajili ya msamaha na urejeshwaji…. Leo anasimama kwenye madhabahu ya uvumba, akimwasilishia Mungu maombi ya wale wanaotamani msaada wake.
Yesu huinua roho zao wanaomgeukia kama kimbilio, juu ya wanaoshitaki na ugomvi wa ndimi za watu. Hakuna mtu au malaika waovu wanaoweza kushitaki roho hizi. Kristo huwaunganisha na tabia yake mwenyewe ya kimbingu. Huwa wanasimama kando ya Mbeba dhambi mkuu, katika nuru inayotoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu.
ZAIDI YA YOTE USITENDE TENA DHAMBI WALA KUURUDIA UOVU WAKO WA ZAMANI IMARIKA NA YEYE ALIYE MWEZA WA YOTE NA AKUSAIDIE
HERI NA UMEBARIKIWA WEWE UMTAFUTAE SANA MUNGU
No comments:
Post a Comment