*WIMBO WA MUSA NA MWANAKONDOO*
*_Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. Kutoka 15:2._*
⚜Kutoka kwenye hatari kubwa, usiku mmoja ulileta ukombozi mkamilifu. Kundi kubwa, lililohitaji msaada – wanaume watumwa ambao hawakuzoea vita, wanawake, watoto na ng’ombe, bahari ikiwa mbele zao na majeshi yenye nguvu ya Misri yakiendelea kuwakaribia kutokea nyuma – umati huu ulishuhudia njia yao ikifunguka kwenye maji na adui zao wakishindwa katika hatua waliyotarajia kushinda. Ni Yehova pekee aliyewaletea ukombozi na mioyo yao iligeuziwa kwake ikiwa na shukrani na imani. Msisimko wao uliwafikishia kwenye nyimbo za sifa.
⚜Roho wa Mungu alikaa juu ya Musa naye akaongoza watu katika wimbo mkuu wa ushindi wa shukrani, moja kati zile za awali na za utukufu mkubwa zaidi zinazofahamika kwa watu…
⚜Wimbo sio wa Wayahudi peke yao. Unaelekeza mbele kwenye maangamivu ya maadui wote wa haki na ushindi wa mwisho wa Israeli ya Mungu. Nabii wa Patmo aliona umati wa watu waliovaa mavazi meupe “wenye kushinda,” nao “walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo” (Ufunuo 15:2,3)…

⚜Wakazi wote wa mbinguni wanaungana katika kumsifu Mungu. Hebu tujifunze wimbo wa malaika sasa, ili tupate kuuimba tutakapojiunga na safu yao inayong’aa.
No comments:
Post a Comment