Tarehe 2/4/2017
*Kwa Walio Uhamishoni*
▶Iwapo ungepewa kipande cha karatasi kinachoanza kwa neno, “Mheshimiwa,” ungetambua kwamba unasoma barua. Na ungedhani kuwa barua ile ilitoka kwa mtu fulani ambaye huenda hukuwa karibu naye.
▶Kama zilivyo barua za kisasa kwamba zina kanuni ya kuanza, ndivyo zilivyokuwa barua zile za kale. Kwanza Petro anaanza kama vile ambavyo mtu ye yote wa kale angelianza. Inamtambulisha mwandishi na wale ambao ilitumwa kwao.
▶Soma 1 Petro 1:1. Tunaweza kujifunza kitu gani kutoka katika aya hii moja ambacho kitatusaidia kupata sehemu ndogo ya muktadha?
▶Petro anajitambulisha kwa uwazi. Jina lake ndilo neno la kwanza katika barua hii. Hata hivyo, mara moja anajitambulisha kama “mtume wa Yesu Kristo.” Kwa hiyo, kama vile Paulo alivyofanya mara kwa mara (Wagalatia 1:1, Warumi 1:1, Waefeso 1:1), Petro mara moja anathibitisha “sifa” zake, akisisitiza mwito wake mtakatifu. Alikuwa ni “mtume,” yaani “mtu aliyetumwa,” na aliyemtuma ni Bwana Yesu Kristo.
▶Petro anatambulisha eneo ambalo barua yake ilielekezwa: Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia. Haya yote ni maeneo ndani ya Asia Ndogo, karibu sawa na eneo la Uturuki ya leo mashariki ya mlango wa bahari wa Bosporus.
▶Zipo hoja kuhusu iwapo Petro alikuwa akiandika zaidi kwa waumini wa Kiyahudi au kwa waumini wa-Mataifa. Maneno anayotumia Petro katika 1 Petro 1:1 “Utawanyiko/wageni,” ni maneno ambayo kwa asili yanawahusu Wayahudi waliokuwa wakiishi nje ya Nchi Takatifu katika karne ya kwanza. Maneno kuteuliwa(BHN) na kutakaswa katika 1 Petro 1:2 yanafaa kwa wote Wayahudi na Mataifa. Kuwaeleza wale ambao wako nje ya jumuia kuwa ni “Mataifa” (1 Petro 2:12; 4:3) pia husisitiza tabia ya Kiyahudi ya wale ambao Petro anawaandikia.
▶Wafasiri wengine wanatoa hoja, kwa kujibu, kwamba kile Petro anachokisema katika 1 Petro 1:18;4:3 kingekuwa sahihi zaidi kusemwa kuhusu waongofu wa Mataifa wanaoingia katika Ukristo kuliko kwa wale wa Kiyahudi. Hata hivyo, je Petro angeweza kweli kuwaandikia Wayahudi kuhusu “mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;”? Au je angeweza kusema kwa wasomaji Wayahudi, “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali” (1 Petro 4:3)?
▶Hata hivyo, kilicho cha maana sana kwetu si nani aliandikiwa, bali, kile ambacho ujumbe unasema.
ππππππππππ
No comments:
Post a Comment