RIA ZA MUNGU (Amri 10)
Hii inaitwa sheria ya Mungu isiyobadilika kwa sababu, Mungu habadiliki badiliki, yaani hana kigeugeu, na maneno yake ni amini. Hes. 23:19, Yak 1:17, Tito 1:2 na 1Sam 15:29
Sifa za sheria za Mungu.
(i) Ziliandikwa na Mungu mwenyewe kwa chanda chake.Kut.24:12, 31:18, Kumb. 9:10
(ii) Ziliandikwa katika mbao mbili za mawe Kut. 31:18
(iii) Zilitunzwa ndani ya sanduku la agano. Kumb. 10:1-2
(iv) Nakala ya sheria hiza iko mbinguni. Uf. 11:19
(v) Zitatumika katika hukumu siku ya mwisho.
Ndizo zitakazokuwa kipimo katika hukumu ya Mungu ijayo
· Yak 2:10-12 - Tutahukumiwa kwa sheria ya uhuru
· Math. 19:16-19 – Ukitaka kuingia mbinguni, zishike amri
· Rum 2:13 – Zishike amri.
“Watakaoingia mbinguni ni wale tu wayafanyao mapenzi ya Mungu,na mapenzi ya Mungu ni kuzishika amri zake. Mith. 7:20, Yoh 14: 15”.
(2).SHERIA ZA MAAGIZO
Kwa uongozi wa roho mtakatifu, sheria hizi ziliandikwa na Musa,na zina sifa hizi:
(i) Mwandishi wake ni Musa (Nabii wa Mungu)
Kumb 31:9
(ii) Ziliandikwa katika chuo/magombo/magome ya miti yaliyotengenezwa kwa ustadi. Kumb. 31: 24
(iii) Zilihifadhiwa kando ya sanduku la agano lililokuwa na amri kumi (10) za Mungu. Kumb. 31: 26.
Sheria za maagizo zilihusu mambo haya:
(a). Tohara (Mwanzo 17:9-11)
Sheria hii ilifikia ukomo wake, kwani ilikuwa ni mfano kivuli. 1Kor. 7:19, Rum 2: 28-29
(b). Kafara ya wanyama (Walawi 16:15)
Sheria hii ilifika ukomo pale msalabani kwa sababu ya kafara ya Yesu Kristo, Luka 23:44, 45, 1Yoh. 1:7, Rum 5:9, 1Pet 1:19
(c). Ndoa (Walawi 18:20-22)
Sheria hii inaendelea. Ebr. 13:4, Kut. 20:14
(d). Mavazi (Kumb. 22:5)
Sheria hii inaendelea. 1Tim 2:9
(e). Afya (Walawi 11, Kumb.23:12-14)
Mungu anahitaji tule kilicho chakula (walawi 11) na kuyaweka mazingira safi (kumb. 23:12-14)
Sheria hii inaendelea. (1Kor.3:16-17, 6:19-20
(f). Zaka na sadaka (Walawi 27: 30-34)
Twapaswa pia kulitekeleza agizo/ amri hii. Malaki 3:10
(g). Sikukuu (Walawi 25)
Ziko sikukuu zilizofikia ukomo na zingine zinaendelea. Mf. Isaya 66:22-23, kut. 31:12,17, Ezek 20:12, kumb. 16:13-19, Zek. 14:16
KAZI YA SHERIA NI KUKUONYESHA KUA UMEKOSEA AU LA
No comments:
Post a Comment