Pages

Saturday, 8 April 2017

KESHA LA ASUBUHI Tabia Mbaya Kabisa ya Kishetani

*🌹KESHA   LA  ASUBUHI🌹*
J'PIL. April: 9/2017



*Tabia Mbaya Kabisa ya Kishetani*


*👉🏽📖“Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu” (Mithali 27:4)..*


*✍🏽📚.Shutuma za Miriamu na Haruni zilivumiliwa na Musa katika utulivu bila kulalamika. Ulikuwa ni uzoefu uliopatikana wakati wa miaka ya taabu na kungojea akiwa huko Midiani—ambapo tabia ya unyenyekevu na uvumilivu ilijengewa—ndipo Musa alipojiandalia ili kukabiliana na hali ya kutoamini na manung’uniko ya watu hawa na kiburi na chuki ya wale ambao wangepaswa kuwa wasaidizi wake thabiti. Musa “alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi,” na hii ndiyo sababu alipewa hekima na uongozi wa kiungu kuliko wengine wote. Maandiko yanasema, “Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake” (Zab. 25:9). Wapole huongozwa na Bwana, kwa sababu wao hufundishika, wakiwa radhi kuelekezwa…..*




*✍🏽📚“Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu.… Hasira za Bwana zikawaka juu yao; Naye akaenda Zake.” Kisha lile wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema kama ishara ya ghadhabu ya Mungu, na Miriamu akaadhibiwa. Alipatwa na “ukoma, mweupe kama theluji.”… Sasa kiburi chao kikashushwa mavumbini, Haruni akaungama dhambi yao, na akasihi kwamba dada yake asiachwe aangamie kwa kisasi hicho cha kuchukiza na kufisha. Katika kuyajibu maombi ya Musa, ukoma wake ukaponywa. Hata hivyo, Miriamu alifungiwa nje ya kambi kwa muda wa siku saba….*




*✍🏽📚Udhihirisho wa ghadhabu hii ya Mungu ulikusudiwa kuwa onyo kwa Israeli wote, ili kuzuia roho ya kutoridhika na kutotii iliyokuwa ikizidi kuongezeka. Kama chuki na kutoridhika kwa Miriamu visingekaripiwa waziwazi kiasi hicho, vingesababisha uovu mkubwa. Chuki ni mojawapo miongoni mwa tabia mbaya mno za kishetani ambazo zinaweza kudumu moyoni mwa mwanadamu, na ni mojawapo yenye matokeo maovu sana kuliko zote…. Ilikuwa chuki ndiyo ambayo hapo awali ilisababisha machafuko mbinguni, na uendekezaji wa tabia hii umesabaisha maovu yasiyohesabika miongoni mwa wanadamu. “Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya” (Yakobo 3:16).13*



______________________________


*TAFAKARI    NJEMA*

No comments:

Post a Comment