Pages

Thursday, 6 April 2017

MAJARIBIO SABA YA MWENENDO WETU PAMOJA NA MUNGU.

MAJARIBIO 7 YA MWENENDO WETU PAMOJA NA MUNGU.

Na Mwinjilist Deodatus chaula(Punda wa Yesu).

    siku ya Kwanza.
*Jijaribuni wenyewe,Kwamba Mmekuwa katika imani,Jithibitisheni wenyewe.* 2Kor 13:5

Mpendwa Taifa la Mungu nakusalimu Kwa Jina La Yesu Kristo wa Nazareth. Namuomba Mungu Roho Mtakatifu Akufundishe katika Mfululizo wa Somo hili Mpaka litakapo isha usikate tamaa kusoma.

Majaribu ni Mitihani ambayo Mtu hupewa na Mungu,Mwanadamu,Au ibilisi. Majaribu yanaweza kuja katika ubaya lakini yakawa yamebeba Mema. Yanaweza kuja kwa uzuri yakawa yamebeba ubaya. Hivyo Katika kila safari yetu tunamuhitaji Yesu atufundishe nia ya kila Jaribu Mbele Zetu.

Sisi kama tuliookoka ili Mungu apate kutuamini ,Apate Kujivunia Uwepo wetu hapa duniani lazima tupite baadhi ya mitihani iletwayo na Mungu,Au Ibilisi. Au mitihani ya wanadamu.

Kwa Neema Za Mungu Mungu amenijalia Kunifundisha Majaribu 7 Ambayo kila Mkristo. Inapaswa Ajiangalie,ajichunguze,ajitathmini kama kweli yupo na Mungu au hayupo na Mungu bali anaMungu wa Mapokeo.

Sikia hapa sizungumzii dhehebu unalo sali,unaweza kuwepo kwenye kanisa lenye nguvu za Mungu,ila Wewe usiwe na nguvu za Mungu. Maana sio kila anaye fanyia Bank ni tajiri. Wengi wao ni maskini.

Unaweza kuwepo kwenye kanisa Takatifu ila wewe usiwe mtakatifu na ukaingia Motoni kabisa. Maana sio kila Asomeaye Uchumi ni mchumi.

Unaweza Ukawa umebatizwa kwa maji Mengi,ukaingia Mbinguni,au unaweza kuingia Motoni na ukateseka huko.miaka Yote. Unaweza ukabatizwa kwa majinmachache na ukafika Mbinguni vizuri.

Jaribio la Kwanza.

KUENENDA NURUNI.
*Tukisema kwamba twashirikiana naye(Mungu wa Nuru) tena tukienenda gizani twasema uongo,wala hatufanyi iliyo kweli*(1Yohana 1:6).

Mungu ni Nuru,Mwanga,Anatutaka nasi tuwe nuru,tuwe chumvi,tuwe chanzo cha Mabadiliko. Tuwe taa gizani. Siku hizi. Ni shida tuu. Utasikia mtu anasema ameokoka na anaubaguzi ,unawapenda watu wa kanisa / dhehebu lako tu. Unadhani Yesu angewapenda watakatifu tuu,na je Mimi leo ningeweza kumjua ??. Unadhani pasipo kuwapenda waendao katika njia za uovu watapataje kuijua kweli??.

Wengi wetu tunaishi kwa unafiki sana,mchana ni Watoto wa Mungu usiku sio. Walokole siku hizi wanaongoza kwa majungu,unafiki,masengenyo,wizi. Umalaya tupo,hatuna upendo wa kweli bali upendo wa ubaguzi kuwapenda waliookoka tu. Hapo sio nuruni tena bali gizani.

Ninakasirika sana kukutana na wapendwa waliokatishwa tamaa na sisi watumishi,walokole. Tumewavunja mioyo kweli wenye imani changa. Naomba Ubadilike uwe Kwelu mbele za Mungu.

2. Jaribio la Pili.

KUBALI U MWENYE DHAMBI.

Biblia inasema Tukisema hatuna dhambi,twajidanganya wenyewe,wala kweli haimo ndani yenu.(1Yohana1:8).

Huwezi kutembea na Mungu huku unatenda dhambi. Mungu anae delea kutuonyesha dhambi zetu mara kwa mara.. Lakini tukiziungama,na kutubu dhambi zetu mbele za Mungu Yeye hutusafisha..

Kadiri uanavyokua kiroho ndivyo utakavyozidi kufunuliwa dhambi nyingi ambazo zimejificha ndaninya Moyo wako ambazo hazikuonekana Mwanzo. Mwambie Mungu akusafishe Kabisa.

3. Jaribio la Tatu.

TII MAPENZI YA MUNGU.

Biblia inasema Yeye asemaye nimemjua wala hazishiki amri zake,ni Mwongo wala kweli haimo ndani yake( 1Yohana 2:4). Hakuna jaribio kubwa duniani kama jaribio la Utii kwa Mungu,wazazi,sheria,viongozi. Na wazee wetu. Utii kwa wanadamu wenzetu. .

Aliye Mkristo wa Kweli ,humtii Mungu. Na kumtii Mungu ni kushika amri za Mungu. Na Amri za Mungu ndio hizi. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,roho yako,akili zako zote,na jirani yako kama nafsi yako.

Huwezi sema unampenda Mungu huku ukitumia Muda mwingi kuangalia senema za kidunia kuliko kutafakari Neno la Mungu. ,Unafowad meseji za ajabu na huku jumbe za Mungu unaziacha. Unachati messji za ajabu unaacha kumtangaza kristo.

Unatoa michango mikubwa kwenye harusi,send off,ila sadaka kidogo,kuchangia huduma za Mungu kwa watumishi umekuwa bahili. Hu mpendi Mungu kabisa. Maana bado unaishi kisheria nasio kiroho....

Hauna utii kwa neno la Mungu,hauna utii kwa mumeo,mkeo,wadogo zako. Heshima huanzia kwa mkubwa na hushuka kwa walio wadogo zako. Mchungaji / mwinjilist,nabii unataka waumini wakutii wakati wewe hauna utii kwao,watajifunza toka wapi,unahubiri upendo wakati wewe hauna upendo ni kazi bure.

Mkinipenda mtazishika amri zangu,tena ninyi mmekuwa rafiki zangu,mkitenda niwaamuruyo.( Yohana15:14). Haya nawaamuru ninyi mpate kupendana( Yohana 15:17).

4. Jaribio la nne.

MWIGE KRISTO YESU KRISTO.

ukitaka kuwa mkristo Tafuta kujua sana Kristo aliishije,alikuwa anatumiaje muda wake,alikuwa anaombaje,anahubirije,anaishije na mafarisayo,wenye dhambi aliishije nao,walevi nao aliishije. Kwa nini huduma ndani ya Yesu Ilikuaje,kwa nini ilikuwa na nguvu vile. Malengo ya Yesu yalikuwaje. Mavazi yake,tembea zake,nyoa zake ,semi au maneno yeke kinywani yalikuwaje. Utabadilika na kuanza kumfuata katika kila hatua. Kwa nini akiaamua kujitesa kwaajili yangu na yako??.

Biblia inasema Yeye asemaye anakaa ndani yake,imempasa Yeye kuenenda vile vile kama yeye alivyoenenda( 1Yohana 2:6).
Chumvi hufanya radha ya chakula kuwa nzuri,hivyo kuongeza hamu ya kula chakula. Pasipo chumvi chakula hakiwezi kuliwa. Je wewe umefanyika chumvi kwa wengine wamjue Mungu??. Chumvi huvuta Maji,sehemu ilipo. Hufanya kiu ndani ya mtu. Ili aweze kunywa maji. Mimi na wewe kama chumvi lazima uwe na kiu ya watu wengine wamjue Kristo. Nawe we ukijibidiisha kumjua zaidi Mungu.

Kwa leo naomba Niishie Hapa. Mungu akupe wepesi wakuelewa kwa kina nini maana Ya Kristo ,Misingi ya Kristo. Mkristo ni nani? Na mpagani ni mtu gani. Ni wapi au lini sifa za mkristo huvuliwa.

Au uanachama wako kwa Kristo huvuliwa na kuwa chama cha upinzani. Sikia kuzaliwa kwenye familia ya WanaCCM( chama cha siasa Tz) haikupi sababu ya wewe kuwa mwanachama wa CCM daima. Muda wowote unaweza kuvuliwa uanachama kwa usaliti wako. Ndivyo ilivyo kwa Kristo usipo fuata sheria zake,amri zake,Tabia zake wewe sio Mkristo.

Sikia Hii Yesu alisema Watu hawa huniabudu kwa midomo yao tu,ila Mioyo yao ipo mbalu sana nami. Hawa nao sio wakristo. Tu ahitaji toba ya kweli.

Forward ujumbe huu kwa watu wote ulio na namba zao nao wapone,Wamjue Kristo zaidi Mungu akubariki kwa kujitoa sadaka hiyo kuu.

By. Mtumishi wa Yesu Kristo( Punda wa Yesu

No comments:

Post a Comment