Pages

Thursday, 6 April 2017

BIBLIA KULEA WATOTO

BIBLIA KUWALEA WATOTO VEMA

Ni wajibu wa wazazi kuwalea watoto vema katika maadili mema, tabia njema na katika imani bora
watoto walio kua katika imani ni watoto wenye hofu ya MUNGU huwa ni watii na wanyeyekevu sana kushinda wale ambao awaja lelewa katika imani
wazazi bora uwatunza watoto wao kiafya, kifikra, na kiimani
je biblia inatuambiaje soma mafungu yafuatayo
*~~MITHALI 22:6*
Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

*~~WAEFESO 6:4*
Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana

*~~MITHALI 22:15*
Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

*~~MITHALI 13:24*
Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

*~~MITHALI 19:18*
Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.

*~~MITHALI 23:13*
Usimnyime mtoto mapigo; kwa maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

MLEE MTOTO KATIKA KUYATUNZA YALIYO MEMA NAYE MUNGU ATAKUPA UJIRA WAKO USIMCHUKIE MWANAO ANAPO KOSEA BALI MWONYE KIKAMILIFU NA KUMWADHIBU AKOSEAPO NI KUMJENGA SI KUMWARIBU

*WAZAZI NA WALEZI TIMIZENI WAJIBU WENU, ACHENI KUDEKEZA WATOTO, MTAKUJA KULIZWA NA WATOTO WENU*

No comments:

Post a Comment