Kuishi Maisha ya Wokovu
Soma 1 Petro 1:13-21. Kwa mujibu wa kifungu hiki, ni kitu gani kinapaswa kuhamasisha tabia ya Kikristo?
Neno kwa hiyo, ambalo huanza 1 Petro 1:13 linaonesha kwamba kile ambacho Petro atasema baada ya hapo hutokana na kile ambacho amekuwa akikiongelea punde tu. Kama tulivyoona katika somo la jana, Petro alikuwa akizungumza juu ya neema ya Mungu na tumaini walilo nalo Wakristo katika Yesu Kristo (1 Petro 1:13-21).
Kama matokeo ya neema na tumaini hili, Petro anawasihi wasomaji wake kwa kusema “ vifungeni viuno vya nia zenu” (1 Petro 1:13). Yaani, kama itiko kwa wokovu walio nao katika Yesu, ni lazima waandae akili zao ili wapate kusimama imara na kuwa waaminifu (1 Petro 1:13).
Soma 1 Petro 1:13. Ina maana gani kuweka tumaini lako kikamilifu juu ya neema iliyodhihirishwa katika Yesu?
Hakuna swali, Petro anawaambia kuwa matumaini yao yapo katika Yesu peke yake. Ndipo anasisitiza kuwa kiwango fulani cha tabia kinatarajiwa kutoka kwa Wakristo kama matokeo ya wokovu wao. Anabainisha vitu vitatu vikubwa katika kuhamasisha tabia ya Kikristo: tabia ya Mungu (1 Petro 1:15, 16), hukumu ijayo (1 Petro 1:17), na gharama ya ukombozi (1 Petro 1:17-21).
Jambo la kwanza ambalo litahamasisha tabia ya Kikristo ni tabia ya Mungu. Tabia hii inaweza kuwekwa pamoja kwa njia hii: Mungu ni Mtakatifu. Petro ananukuu kutoka Mambo ya Mambo ya Walawi 11:44, anaposema, “Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” (1 Petro 1:16). Kwa hiyo wale ambao wanamfuata Yesu pia lazima wawe watakatifu (1 Petro 1: 15-17).
Kitu cha pili kinachohamasisha tabia ya Kikristo hupatikana katika utambuzi kwamba Mungu, ambaye ni mtakatifu, atamhukumu kila mtu bila upendeleo, kwa mujibu wa kile ambacho kila mtu amefanya (1 Petro 1:17).
Kitu cha tatu kinachohamasisha kinatokana na ukweli mkubwa kwamba 1 Wakristo wamekombolewa. Hii ina maana kwamba 2 wamenunuliwa kwa bei kubwa, bei ya juu sana: damu ya thamani 3 ya Kristo (1 Petro 1:19). Petro anasisitiza kuwa kifo cha 4 Yesu hakikuwa ajali ya historia bali ni kitu 5 kilichowekwa imara kabla ya misingi ya ulimwengu (1 Petro 1:20).
Ni kitu gani kilichokusukuma wewe kuwa Mkristo? Ungejibu, nini na kwa nini, kama mtu angekuuliza, Kwa nini wewe ni Mkristo? Leta majibu yako katika darasa siku ya Sabato.
No comments:
Post a Comment