Pages

Thursday, 6 April 2017

KESHA LA ASUBUHI

       *🌻KESHA    LA   ASUBUHI🌻*
                                                                       *Njia Salama*

📖BWANA  akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. Kutoka 14:15.*

               🌹🌺🌹🌺🔛🌹🌺🌹🌺

*📚✍🏽 Kutokana na uwezo wake wa kuona mbali {👁👁}, Mungu aliwaleta Waebrania hadi kwenye ngome ya mlima kabla ya bahari, ili apate kuwaonesha nguvu yake katika ukombozi wao na aoneshe dhahiri ishara ya kushusha kiburi cha watesaji wao. Angeweza kuwaokoa kwa njia nyingine yoyote, lakini alichagua njia hii ili pia apate kuijaribu imani yao na kuimarisha tumaini lao kwake. Watu walikuwa wamechoka na kuogopa, na bado ikiwa wangebaki pale Musa alipowaambia waendelee mbele, Mungu asingefungua njia kwa ajili yao. Ilikuwa hivi: “Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu” (Waebrania 11:29). Kwa kutembea wakielekea kwenye maji, walionesha kwamba waliamini neno la Mungu kama lilivyonenwa na Musa. Walifanya yale yote waliyoweza kufanya na kisha Mwenye nguvu wa Israeli akayagawa maji ili kufanya njia kwa ajili ya miguu yao.*

*📚✍🏽Fundisho kuu lilitolewa hapa ni kwa ajili ya wakati wote. Mara kwa mara maisha ya Kikristo hushambuliwa kwa hatari na inaonekana kuwa vigumu kutekeleza majukumu. Fikra inaonesha uangamivu ulio mbele na utumwa au kifo nyuma. Licha ya hayo, sauti ya Mungu inanena kwa uwazi kabisa, “Endelea mbele.” Inatupasa kuitii amri hii, hata kama macho. yetu hayawezi kupenya kwenye giza na tunajisikia mawimbi ya baridi chini ya miguu yetu. Kamwe vikwazo vinavyozuia maendeleo yetu havitatoweka mbele ya roho inayosita sita, yenye mashaka. Wale wanaoahirisha utii hadi kila kivuli cha mashaka kitakapotoweka na pasiwepo hatari yoyote ya kuanguka au kushindwa, kamwe hawatatii hata kidogo. Kutoamini kunanong’ona hivi: “Hebu tungoje hadi vizuizi vyote vitakapoondolewa na tuweze kuona njia yetu waziwazi:” lakini kwa ujasiri, imani inatia moyo kwa ajili ya kusonga mbele, ikitumaini yote, ikiamini yote.*

*📚✍🏽 Lile wingu.. {☁} ambalo lilikuwa ukuta wa giza kwa Wamisri lilikuwa mafuriko ya nuru kwa Waebrania, likiangaza kambi yote na kuwapa nuru kwenye njia yao. Hivyo matendo ya Mungu huwaletea wasioamini, giza na kukata tamaa, wakati huo huo, kwa nafsi inayomtumainia, hujazwa na nuru na amani. Njia ambayo Mungu anaongoza kwayo, njia inaweza kupitia kwenye jangwa au bahari, lakini ni njia salama.*


                                                💐💐💐💐🔚💐💐💐💐

             *Je.... Njia uifuatayo ni sahihi kwa ajili ya wokovu wa maisha yako...?*..

                                                 TAFAKARI NJEMA..

No comments:

Post a Comment